Kuhusu NIJUZE TECH
Tunaamini kila mtu anaweza kujifunza teknolojia na kuitumia kubadilisha maisha na biashara yake.
Jukwaa la kujifunza na huduma za kidijitali
NIJUZE TECH ni jukwaa la kujifunza na kupata huduma za kisasa za kidijitali. Tunafundisha kwa lugha rahisi na mifano ya vitendo jinsi ya kutumia zana za AI kutengeneza video, kuhariri video kwa CapCut, kubuni graphics kwa Canva, kujenga website na kutangaza biashara mtandaoni.
Mbali na mafunzo, tunatoa huduma kwa biashara zinazohitaji website, maudhui ya mitandao ya kijamii na kampeni za matangazo.
Hadi sasa tumewasaidia wanafunzi zaidi ya 600 kujifunza ujuzi wa kidijitali (digital skills), na tumeendesha akaunti za matangazo ya kulipia zenye bajeti ya zaidi ya milioni 5.
Dhamira Yetu
Kuwawezesha vijana, wajasiriamali na wabunifu kupata ujuzi wa kidijitali unaowasaidia kujiajiri, kuajiriwa na kukuza biashara.
Maono Yetu
Kuwa kitovu kinachoaminika cha kujifunza teknolojia na ubunifu kwa Kiswahili.
Tunachosimamia
Urahisi
Tunafundisha hatua kwa hatua kwa lugha inayoeleweka.
Vitendo
Kila somo lina mfano wa kazi halisi unayoweza kuifanya.
Uaminifu
Tunaeleza ukweli kuhusu uwezo na mipaka ya kila zana.
Kusasisha
Teknolojia hubadilika; tunasasisha mafunzo yetu mara kwa mara.

